Adam Zakaria Kinyekire: Mtanzania aliyetengeneza helikopta aunda gereji la kuhama hama linalohudumu hadi Zambia.

 

Adam ndiye mtanzania aliyetengeneza helkopta kupitia gereji yake ya ufundi. Adam anasemema kuwa mara baada ya kumaliza shule ya msingi alianza kujifunza kutengeneza magari katika karakana ya kawaida.
Adam Alijifunza kazi hiyo mwenyewe bila kuhudhuria chuo chochote, lakini ni maarufu kwa kuunda helikopta na pia amewafurahisha madereva kwa gereji lake la kuhama hama. Kwa sasa anafanya kazi na vijana takribani 40 na wengine zaidi na 50 walipitia katika mikono yake kupata mafunzo

Adam anasema yeye ni mbunifu ambaye hakupata ujuzi wowote kutoka shuleni maana mara baada ya kumaliza shule ya msingi, alianza kujifunza kutengeneza magari katika karakana ya kawaida na baadaye akaanza kuunda vitu kama vile mashine ya kusagia nafaka, gari la karakana na hata helikopta.
Hii ni nukuu ya Adamu akielezea siri yake kubwa , “Ubunifu wa kutengeneza vitu mbalimbali huwa sifundishwi na mtu ni kitu tu ambacho kipo kwenye damu, ni kama vile ndoto tu ambapo vitu vinakuja kwenye akili kwamba naweza kutengeneza hiki na hiki lakini sijawahi kupata mafunzo popote,” Adam Zakaria anaeleza.
Kwa kusoma habari kamili.
Chanzo cha Habari./ Soucrce of news. https://www.bbc.com/swahili/habari-46265121